NISHA BWANA MPYA, GARI MPYA

Mwaka huu umekuwa wa mafanikio kwa msanii wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ kutokana na kuvuta ndinga mpya na huku akidaiwa kutoka na mwanaume mpya.
Kikizungumza na Ijumaa, chanzo ambacho ni jarani wa msanii huyo kilisema licha ya Nisha kuendesha mkoko huo aina ya Toyota Harrier, sasa anatoka na mwanaume mwingine ambaye mara kadhaa wamekuwa wakimbonji pamoja.
“Sasa ana mwanaume mwingine, huenda ndiye aliyemnunulia lile gari analoendesha,” alidai jirahi huyo wa Nisha.
Nisha alipotafutwa kuzungumzia hilo alisema, ni kweli ana gari lingine ila kuhusu mwanaume anayetembea naye kwa sasa ni siri yake ila atamuanika siku si nyingi kwa kuwa wana mipango mikubwa baadaye.

0 comments:

Post a Comment