MUIGIZAJI wa ‘long time’ katika tasnia ya filamu Bongo, Brandina
Chagula ‘Johari’ juzi kati amefunguka kuwa kwa sasa hayuko na aliyekuwa
akidaiwa kuwa ni mpenzi wake, Vicent Kigosi ‘Ray’ ila yuko katika
Kampuni ya RJ ambayo wanashirikiana kisanii zaidi.
Akizungumza na Ijumaa katika hoteli ya Johannesburg, Sinza Mori
jijini Dar, Johari alisema kuwa kwa sasa angependa atambuliwe kuwa
anafanya kazi na Ray katika hiyo kampuni na si kuhusishwa naye
kimapenzi.
“Naomba ifahamike kwamba mimi niko RJ na siko na Ray kama
watu wengi wanavyozungumza,” alisema Johari kwa kifupi kisha kuendelea
na hamsini zake.
0 comments:
Post a Comment