DUDE AWATOA NISHAI BONGO MUVI.


STAA wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amewatoa nishai viongozi wa Bongo Muvi kwa kueleza kuwa, risala iliyosomwa siku ya ‘bethidei’ yao ya kutimiza miaka mitatu imepotosha ukweli.
Staa wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Dude alisema ameshangaa kusikia kwenye risala hiyo kuwa waanzilishi wa umoja huo ni Kanumba, Sajuki, Jimmy Mafufu na wengineo wakati ukweli hauko hivyo.
“Ile risala imepotosha, Bongo Muvi ilianzishwa na wasanii wa muziki na filamu wakiwemo mimi,  William  Mtitu, H.Baba, Simon Mwakifwamba, MwanaFA na Fid Q na wengineo kwa lengo maalum, nimeshangaa kusikia vile,” alisema Dude huku akisisitiza kuwa, yeye hajisifii ila ukweli usipindishwe.

0 comments:

Post a Comment