Wapo
ambao wakati wanapofanya mapenzi badala ya kupata raha, husikia
maumivu, mwanaume katika uume lakini ni mara chache sana kulinganisha na
wanawake. Mwanamke ndiye husumbuliwa zaidi na tatizo hili.
Mwanamke anaweza kukosa raha kabisa na matokeo yake kuumia wakati
tendo linapoanza pale mwanzoni ukeni au kwa ndani zaidi. Maumivu haya
pia yanaweza kugawanyika katika makundi mawili. Kwanza ni maumivu wakati
wa tendo ambayo ndiyo hayo tuliyoyaona hapo juu na maumivu baada ya
tendo.
Kuumia wakati wa tendo
Maumivu haya hutokea pale uume unapoanza kuingia ukeni na hutokana na uke kuwa mkavu.
Hili linaweza kusababishwa na maandalizi duni kabla ya tendo, matatizo
katika mfumo wa homoni au kupoteza msisimko na hamu ya tendo.
Kubana kwa misuli ya uke pia huchangia ingawa tatizo hili zaidi ni la
kisaikolojia kutokana na mwanamke kuwa na woga wakati wa tendo.
Kuwa na makovu ukeni kutokana na athari za kukeketwa, uwepo wa
michubuko na vidonda au maambukizi ukeni mfano fangasi ya muda mrefu na
maambukizi mengine hasa magonjwa ya ngono.
Uvimbe ukeni au uwepo wa
jipu na vipele, kuumia kwa kufanyiwa vipimo au baada ya kuzaa kwa njia
ya kawaida endapo hukupona vizuri.
Kuhisi maumivu baada ya tendo
Maumivu haya
hutokea muda mfupi baada ya tendo la ndoa. Mwanamke huhisi maumivu kwa
ndani zaidi ukeni au chini ya tumbo. Maumivu huwa makali na huchukua
muda mrefu.
Maumivu ya chini na ndani zaidi ukeni huleta hisia kama
muwasho mkali wa pilipili au kama unakatwakatwa na viwembe na ukinawa
unazidi kupata maumivu.
Maumivu ya ndani zaidi ukeni wakati mwingine huambatana na hali ya
kuhisi kama kuna kitu kinasukumwa wakati wa tendo na unapomaliza tendo
ukinawa unahisi kitu kimevimba ndani ukeni kama kigololi. Maumivu huwa
chini ya tumbo na wakati mwingine husambaa kulia na kushoto ya mirija.
Wengine huumwa na kiuno hata kutembea inakuwa shida mara tu baada ya
kumaliza tendo.
Hali ikiwa mbaya mwanamke hutokwa na damu baada ya tendo, hali ambayo
siyo dalili nzuri kwani hata saratani ya shingo ya uzazi nayo huonyesha
dalili hii ya damu.
Hali ya maumivu pia huambatana na kutokwa na majimaji ukeni wakati
mwingine yakiambatana na muwasho mkali na harufu. Hata wanaume wanaweza
kutokwa na damu baada ya tendo badala ya manii.
Nini cha kufanya?
Tatizo hili ni kubwa na lina
vyanzo vingi kama tulivyoona, hivyo ni vema kufanya uchunguzi kujua
chanzo halisi ndiyo tiba ifuate.
Epuka kutumia dawa bila ya kujua chanzo halisi.
Uchunguzi hufanyika katika hospitali za mikoa, wilaya kwa madaktari wa magonjwa ya kinamama.
Ni vema uwahi hospitali.
0 comments:
Post a Comment