Stori: MAYASA MARIWATA
MWANAMUZIKI Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amesema yupo kwenye
mikakati ya kufunga pingu za maisha na mpenzi wake anayejulikana kwa
jina la Siwema baada ya kumtundika mimba.
Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Nay alisema anajivunia
kukaribia kuitwa baba na kizuri ni kwamba msichana aliyempa mimba
alikuwa na ndoto za kumuita mke wake hivyo ndoa itafungwa kabla ya mtoto
kuzaliwa.
“Kikubwa naomba Mungu mipango yangu iende kama nilivyopanga kwa
sababu nataka kabla mtoto hajazaliwa tuwe ni wanandoa tunaotambulika kwa
Mungu kwa kufunga pingu za maisha,” alisema Nay.
Akizungumzia
kubebeshwa mimba na msanii huyo, Siwema aliliambia Ijumaa: “Najisikia
furaha sana kumbebea mimba Nay, tumetoka mbali naamini ndoto yetu ya
kuoana itatimia siku si nyingi.”
0 comments:
Post a Comment