MAMA ADAI KUIBIWA MTOTO LEBA.


Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jinala Shakila Bakari (30),mkazi wa Mbagala jijini Dar, ametoa madai mazito kuwa manesi wa hospitali moja (jina linahifadhiwa) iliyopo Mbagala wamemuiba mmoja wa watoto wake wawili aliojifungua Machi 28, mwaka huu.

Akizungumza na gazeti hili juzi, Shakila alisema siku ya tukio majira ya saa 6 mchana,alijifungua mtoto wake wa kwanza,lakini kukatokea hitilafu ndogo ya mwanaye huyo kukatwa kidogo na mkasi uliosababisha jeraha kwenye paji la uso.
“Waliniambia walimgusa kidogo kwa bahati mbaya na mkasi, lakini wakasema hakuna tatizo, waliniwekea kifuani na damu ikawa imenivujia kidogo, baadaye nilijisikia uchungu tena, manesi wakamtoa mtoto yule kifuani kwangu ili nipate nafasi ya kujifungua tena, nilipojifungua walinionyesha motto wa kiume,” alidai mama huyo.
Shakila alidai kuwa, tofauti na matarajio yake, alikabidhiwa mtoto aliyejifungua wakati huo huku Yule wa mwanzo akipewa maelezo yasiyoeleweka. “Niliwashangaa manesi. Waliponiona sibabaiki kuhusiana na mtoto wangu ndipo wakaniletea mtoto mwingine wakidai kuwa ndiye huyo. Nilipomchunguza nilibaini kuwa alikuwa wa kiume wakati mimi nilimzaa wa kike, halafu huyu niliyeletewa hakuwa na kijereha.
”Baada ya kumkataa mtoto huyo, Shakila alidai manesi waliondoka na kichanga kile na katika hali ya kushangaza, walisimamia kauli yao ya awali kuwa hakuzaa motto mwingine zaidi ya huyo aliyekuwa naye.
Dada wa Shakila aliyejitambulisha kwa jina la Sikujua Bakari alisemawakati mdogo wake akijifungua yeye pamoja na shemeji yake (mume wa Shakila) hawakuruhusiwa kuingia ndani, lakini baada ya kujifungua walikwenda kumuona akiwa na mtoto mmoja wa kiume, walipompa pongezi walipatwa na mshangao.

0 comments:

Post a Comment