KUMBE! Aliyejipachika kuwa dada wa hiyari wa Mbongo-Fleva, Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye ni zao la Shindano la Kimwana Manywele,
Halima Haruna ‘Kimwana’ amefungukia ishu ya mastaa kibao kujitongozesha
wenyewe kwa jamaa huyo.
Halima Kimwana alielezea sakata hilo wikiendi iliyopita baada ya
kuulizwa undani wa skendo inayomkabili ya kumkuwadia au kumtongozea
Diamond kwa mastaa na kuwabadilisha kama nguo.
Kwa mujibu wa Halima Kimwana, huwa Diamond hajisumbui kumtongoza mwanamke zaidi ya hao mastaa kujitongozesha wenyewe kwake.
Halima Kimwana alidai kwamba yeye kama dada wa mwanamuziki huyo
(hakutaka kufafanua dada kivipi), amefikia hatua ya kusumbuliwa na
wasichana wa kila aina hasa mastaa wakimuomba awatongozee kwa Diamond
tena kwa ahadi kemkemu.
“Kwani unafikiri Diamond anajihangaisha kuwatongoza hao mastaa? Wao
ndiyo kila kukicha wanamsumbua na kutuhangaisha sisi wakitaka
tuwatongozee kwa kaka yetu.
Tena wengine wanatoa ahadi nyingi tu kama tukiwafanikishia,” alisema
Halima Kimwana na kuongeza kuwa katika listi hiyo ya mastaa
wanaojitongozesha kwa Diamond, wapo mastaa wakubwa ambao anawahifadhi
ili asiwavunjie heshima.
Kama hiyo haitoshi, Halima Kimwana alianika kuwa, hajishughulishi na
suala la uhusiano wa Diamond na atamheshimu kila msichana
atakayetambulishwa KAMA WIFI HUKU AKITOLEA MFANO JINSI ANAVYOUHESHIMU
UHUSIANO WA DIAMOND NA WEMA SEPETU KWA SASA.
0 comments:
Post a Comment