HUU NI MSALA!


Kibano! Wanawake wawili, wakazi wa jijini Dar wamekumbwa na bonge la msala baada ya kutiwa mbaroni na kikosi kazi (task force) cha kudhibiti na kupambana na madawa ya kulevya ‘unga’ ambapo wamekamatwa na mzigo huo wenye thamani ya mamilioni ya shilingi, Ijumaa Wikienda limenyetishiwa.
Agness Jerad Musaa.
Taarifa zilizodakwa na gazeti hili kutoka ndani ya jeshi la polisi na kuthibitishwa na kamanda wa kudhibiti madawa hayo nchini, SACP Godfrey Nzowa zilidai kwamba wanawake hao walikamatwa na madawa hayo kwa nyakati tofauti katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar hivi karibuni.
Pamela Kihanira.
Kamanda Nzowa alipozungumza na gazeti hili aliwataja waliokamatwa kuwa ni Agnes Jerald Mussa (42), mkazi wa Magomeni-Mapipa, Dar na Pamela Kihanira  Kibaya (33) (pichani)w, mwenye maskani yake Mbezi-Mwisho, Dar.
Pamela na Agness wakiwa chini ya ulinzi mkali wa makamanda wa Jeshi la Polisi ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar.
Kamanda Nzowa aliweka wazi kwamba Agnes mwenye hati ya kusafiria (passport) namba AB 624446 ya Februari, 2014, alikamatwa Machi 30, mwaka huu, mishale saa 8:30 usiku akijiandaa kupanda ndege kuelekea nchini Uturuki na alikutwa na kilo 1.2 za Cocain zenye thamani ya Sh. milioni 61.5.
Alisema kwamba Pamela mwenye passport namba AB 516016 ya Aprili 12, 2012, yeye alikamatwa Machi 31, mwaka huu, saa 8.00 usiku akiwa na kilo 3.5 za Cocain zenye thamani ya Sh. milioni 179.7 akitokea nchini Brazil.
Kamanda Nzowa aliwashukuru wananchi kwa ushirikiano wa kuwafichua wahalifu hao na amewataka waendelee kutoa ushirikiano kama huo ili kudhibiti biashara hiyo haramu.
Habari za uhakika zilisema kuwa baada ya kuhojiwa na polisi, wanawake hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Aprili 2, mwaka huu ambapo kesi ya Agnes ipo chini ya Hakimu Geni Dudu wakati Pamela ipo kwa Binge Mashabala.Kesi hizo zilitajwa kusikilizwa tena Aprili 16, mwaka huu.
ONYO KUTOKA KWA MHARIRI
Hata kama maisha ni magumu lakini biashara ya unga si ya kufanya kwani ni msala mkubwa pale ndugu, jamaa au rafiki anapokamatwa.

0 comments:

Post a Comment