WOLPER ATESWA MTANDAONI.


STAA wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa anaumizwa na mashabiki wanaomshushia lawama kwa kila anachofanya.
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper.
Akizungumza na paparazi wetu, Wolper alisema wakati mwingine na yeye ni binadamu lakini kila anachokifanya, wafuasi wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakimporomoshea lawama.
“Nashangaa kabisa kuna watu hata ufanye jema wao ni lawama, lakini kimsingi hazinitishi sana maana najua mimi ni staa, wanaonipenda na kuniombea mazuri wapo, nawashukuru wote hata wasionipenda,” alisema.

0 comments:

Post a Comment