Sosi huyo alieleza kwamba Mtitu na wasanii wengine walikuwa wakirekodi filamu ya mwigizaji mwenzake, Sabrina Rupia ‘Cathy’ ambapo Niva alikwenda kuwatembelea hivyo akaombwa gari lake litumike kwa muda wakati yupo hapo.
Ilisemekana kuwa Niva alilala hukohuko, kitendo kilichomshtua mpenzi wake Happy, kwani baada ya kutomuona nyumbani, kesho yake aliamua kumfuata mwanaume wake aliyekuwa ‘location’.
“Sababu ya ugomvi ni Mtitu, naye alienda huko location na bahati akamkuta Niva, akamuuliza kama mpenzi wake huyo alilala huko, kitendo ambacho ilionekana wazi kuwa Mtitu hakupenda kwani alimtishia Niva kuwa atahakikisha amemfukuza kazi mpenzi wake huyo,” alisema sosi huyo.
Sosi huyo alidai kwamba ugomvi ulikuwa mkubwa hadi Mtitu akainua simu na kumwambia Happy asikanyage tena ofisini kwake huku akimtaka Niva kutofika ofisini kwake kwani atavunja gari lake.
Baada ya ushu hiyo kujaa tele kwenye dawati letu, wanahabari wetu walimwendea hewani Niva ambaye alikiri kutokea kwa tatizo hilo na kudai kuwa Mtitu ni mkorofi kwani amekuwa akigombana na kila mtu.
“Mimi ninashangazwa sana na Mtitu kwani ishu binafsi anaziingiza kwenye kazi, sasa amemfukuza kazi mpenzi wangu Happy kisa tu mimi na yeye tulipishana kauli lakini inawezekana kuna kitu nyuma ya pazia ambacho ninakifanyia uchunguzi bado,” alisema Niva.
Kwa upande wake, Mtitu alisema ni kweli alitofautiana na Niva kwani hana heshima kutokana na kumjibu na kumtukana kwa sababu ya mwanamke wake ambaye ni sekretari wake na kuamua kumsimamisha kazi.
“Niva hana heshima halafu ni mtoto mdogo sana kwangu, alinikosea, kuna vitu vibaya alivifanya yeye na huyo mwanamke wake ndiyo maana nimeamua kumsimamisha kazi hadi nikimaliza kushuti ndipo nitakaa na huyo sekretari wangu na kumweleza kinagaubaga kuhusu kuwa na nidhamu kazini,” alisema Mtitu.
0 comments:
Post a Comment