CLOUD AWACHANA WASANII WANAOLIA KINAFIKI MISIBANI

STAA wa filamu Bongo, Issa Musa ‘Cloud’ hivi karibuni aliwachana wasanii wa kike na kuwataka kuachana na tabia ya kulia na kuzimia kinafiki kwenye misiba kwani wanaonesha picha mbaya katika jamii.
Wasanii wa Bongo Muvi na wadau mbalimbali wakiomboleza kifo cha Msanii mwenzao Recho.
Akizungumza siku moja kabla ya mazishi ya aliyekuwa msanii wa filamu, Sheila Haule ‘Recho’, Cloud alisema baadhi ya wasanii wa kike wamekuwa na tabia ya kulia kinafiki kwenye misiba.
“Sitaki kwenye mazishi ya Recho kumuona msanii yoyote akijiangusha baada ya kuona kamera za waandishi eti wamezimia jamani tuwe wastaarabu na kama ukilia uwe unaumia kweli lakini siyo kinafiki kwani wasanii wa kike wamekuwa na tabia ya kujiangusha huku wakiwaomba marafiki zao wawaangalizie simu zao,” alisema Cloud.

0 comments:

Post a Comment