UNATAKA KUMUOA JOHARI? BOFYA HAPA!:

Staa mkubwa wa filamu za Kibongo Blandina Changula "Johari"
Makala: Sifael Paul
Julai 28, 1983 mkoani Shinyanga, alizaliwa mtoto wa kike ambaye sasa ni staa mkubwa wa filamu za Kibongo. Ni maarufu kwa jina

la kistaa la Johari lakini majina yake kamili ni Blandina Changula.

Kama kawaida yetu huwa tunatoa nafasi kwa staa kusimulia alikopitia hadi akafikia mafanikio aliyonayo ili kutoa chansi kwa

Blandina Changula "Johari" akiwa kwenye pozi
wengine kujifunza au kutamani kuwa kama yeye. Yaani kutoka ‘ziro’ hadi ‘hiro’. Leo tunaye Johari kwenye spesho intavyu.

UNGANA NAYE.

Sifael: Johari ni nani?
Johari: Ni staa mkubwa wa Bongo Movies.
Sifael: Elimu yako ni ipi?

Johari: Nimepata elimu yangu ya msingi mkoani Shinyanga katika shule iitwayo Bugoyi.
Nilihitimu mwaka 1996. Baadaye nilipata elimu yangu ya sekondari kwenye shule inayoitwa Buluba kulekule Shinyanga kabla ya

kuja kumalizia elimu yangu kwenye Shule ya Greens ya Dar.

Nilipomaliza kidato cha nne nilisomea mambo ya ‘usekretari’ na baadaye nilisomea mambo ya hoteli hapahapa Dar.

Sifael: Ulianza lini mambo ya kuigiza?
Johari: Nilianza kujiingiza kwenye mambo ya sanaa tangu nikiwa mdogo. Nilianza kuigiza nikiwa shule ya msingi na kanisani.

Nilipenda kuigiza tangu nikiwa mdogo.

Sifael: Ulianza lini kuigiza rasmi?

Johari: Nilianza kuigiza rasmi kupitia Kaole Sanaa Group pale Kigogo, Dar. Nilienda kwa mara ya kwanza kwenye kundi hilo

nikaomba fomu ya kujiunga na kuanza kufanya mazoezi ya kuigiza.

Sifael: Unakumbuka ilikuchukua muda gani wa mazoezi hadi ukaonekana runingani?
Johari: Ilinichukua kama mwaka mzima nikifanya mazoezi na kundi hilo kabla ya kupata nafasi ya kuigiza rasmi kwenye michezo

ya runinga.

Sifael: Ulikuwa na akina nani?
Johari: Nyota yangu ilianza kung’aa nilipokuwa na Steven Kanumba (kwa sasa marehemu) na Vincent Kigosi ‘Ray’ ambao

walinishawishi kuachana na michezo ya runingani na kuanza mchakato wa kufanya filamu.

0 comments:

Post a Comment