UNAMPENDA MTU LAKINI YUPO NA MPENZI WAKE ? BASI UKIFANYA YAFUATAYO LAZIMA UMPATE..CHEKI HAPA:

     


























TUMSHUKURU Mwenyezi Mungu ambaye ametuwezesha kuonana tena tukiwa wazima. Lakini pia tumshukuru kwa kutuletea kitu kinachoitwa mapenzi.Mapenzi yamekuwa yakichukua nafasi
kubwa sana katika maisha yetu ya kila siku na yamekuwa yakichangia kwa kiasi kikubwa furaha kwa kila mtu. 


Kama huamini, angalia wale waliotokea kupenda na wao wakapendwa, utabaini nyuso zao zimetawaliwa na
furaha isiyo na kifani. Lakini mapenzi hayo hayo yamekuwa ni chanzo cha vilio kwa baadhi ya watu.

Mpenzi msomaji wangu, kupenda hakuna macho! Moyo ukishapenda hausikii la kuambiwa. Katika hili ndiyo maana unaweza kumuona mwanaume kazimika kwa demu ambaye hawaendani kabisa lakini moyo wake ndiyo umeshapenda.

Ilishawahi kutokea msichana akampenda kijana mmoja ambaye ni fukara kupita maelezo. Yeye akawa ndiyo anamhudumia kwa kila kitu. Akamfanyia mpango wa ajira na mwisho wake wakafunga ndoa.

Sasa hivi wanaishi maisha ya furaha na amani. Wamegeuka mfano wa kuigwa kwa jinsi wanavyopendana lakini huko nyuma msichana huyo alikuwa akichekwa kwa kutoa penzi kwa mwanaume asiye na mbele wala nyuma.

Hayo ndiyo mapenzi jamani! Lakini pia katika kufurukuta kumtafuta mpenzi wa kuwa naye maishani, mwanaume anaweza kujikuta unaangukia kwa demu ambaye tayari ana mpenzi wake.

Moyo wako unakuambia yeye ndiye mtu sahihi katika maisha yako lakini tayari ana mtu wake, unafanyaje ?.

Utapambana kuhakikisha unapata kile ambacho moyo wako umekipenda au utakubaliana na ukweli kwamba huwezi kuwa naye kwa kuwa ana mtu wake? Inapofikia hatua hiyo unaweza kujikuta upo njia panda hasa pale ambapo huyo mwenye mtu wake naye anaonesha kuwa na chembechembe za mapenzi kwako.
Kuna mambo kadhaa ya kukusaidia kukabiliana na hali hii.

Chunguza. 
Tumia muda wako mwingi kuchunguza juu ya uhusiano wake. Uhusiano wao umesimama na wanaonekana ni watu wenye ‘future’? Nasema hivyo kwa sababu, yawezekana uhusiano wa huyo uliyetokea kumpenda ni wa kuzuga tu na huenda wewe ndiye mwenye ‘future’ naye. Ndiyo maana nikasema chunguza uhusiano wake kwanza.

Usitafute uadui. 
Baada ya kuchunguza, ukibaini kwamba uhusiano wao hauko ‘siriasi’, vuta subira, lolote linaweza kutokea na likaufurahisha moyo wako. Lakini kama utaona ni watu walio siriasi na wanaelekea kuoana, usitafute uadui bure, kaa pembeni.

0 comments:

Post a Comment