MARTIN KADINDA: ‘KUMMENEJI’ WEMA SHUGHULI PEVU


MENEJA wa Wema Isaac Sepetu, Martin Kadinda amekiri kuwa kumsimamia ‘kummeneji’ staa huyo ni shughuli pevu kwani ana tabia ya kubadilika.
Meneja wa Wema Isaac Sepetu, Martin Kadinda akiwa na na Staa huyo.
Alisema Wema anahitahi hesabu kwani kuna vitu unaweza kupanga naye lakini akashindwa kutimiza kutokana na hisia zake binafsi.
“Kuna wakati unaweza kumwambia usitoke hadi nikuruhusu lakini cha ajabu unakuja kushtukia mwenzio yupo mtaani jambo ambalo hamkukubaliana, ni ngumu we’ acha tu,” alisema Martin Kadinda ambaye pia ni mbunifu wa mavazi.

0 comments:

Post a Comment